App hizi zitakupa urahisi sana wa kupata filamu yoyote, tamthilia (series) mbalimbali pamoja na kuwa na uwezo wa kuangalia trailer au hata filamu hizo moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi. Najua leo ndio siku yako ya kupumzika basi bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi nzuri.
TeaTV ni app ya kwanza kwenye list hii app hii intakupa uwezo wa kupakua filamu, series na hata tamthilia kwa haraka sana. App hii ni rahisi sana kutumia na inapatikana bure kabisa. Unaweza kupakua app hii kwa kubofya link hapo chini.
DOWNLOAD TEA TV
The Movie DB ni appa nyingine nzuri sana ya kudownload movie na series, application hii itakupa uwezo wa kuchagua kulingana na mwaka, genre na pia tofauti na app iliyopita, App The Movie DB inayo sehemu ya filamu za katuni hivyo utaweza kudownload filamu za katuni (Animation) kwaajili ya yako au hata watoto wako. Kama kawaida link ya kupakua App hii iko hapo chini.
DOWNLOAD THE MOVIE DB
Show Box ni Application nyingine bora kabisa kwaajili ya kudownload filamu, Application hii itakupa uwezo wa kupakua filamu, na tamthilia moja kwa moja kupitia sim yako ya Android. Kingine kiziri kuhusu App hii ni kuwa itakupa uwezo wa kusoma habari mbalimbali zinazohusiana na filamu mpya na hata zile zinazokuja huku ikikonyesha na Trailer za filamu hizo.
DOWNLOAD SHOW BOX
Popcorn time ni app nyingine nzuri sana kwaajili ya kupakua filamu, kupitia App hii utaweza kupata movie mpya kulingana na umaarufu wake. Mbali na movie pia utaweza kudownload series pamoja na animation moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.
DOWNLOAD POPCORN TIME
Terrarium tv ni app nyingine nzuri sana kwaajili ya kupakua filamu, app hii nimekuwa nikitumia kwa muda mrefu sasa na kweli imekuwa ikinisaidia sana kupata filamu kwa wakati. App hii inakupa filamu na tamthilia mpya na uzuri ni kuwa kila filamu mpya itakapo kuwa inapatikana kupitia App hiyo basi utatumiwa ujumbe moja kwa moja ili uweze kupakua. Muhimu ni kuwa kumbuka kufuata hatua za muhimu ambazo tulionyesha kwenye makala iliyopita ili kupata filamu yenye muonekano mzuri, unaweza kuangalia video hapo chini kujua jinsi ya kutumia.
0 Comments